Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya kabla na baada ya uchaguzi mkuu, inatarajiwa kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Alhamisi ya Aprili 23, 2026 ikiwa ni siku moja kabla ya muda iliyoomba kukamilisha uchunguzi wake.
Hatua hiyo, inakuja ikiwa ni miezi mitano tangu tume hiyo ilipoundwa Novemba 18, 2025 na Rais Samia kuchunguza undani wa sababu na chanzo cha matukio ya maandamano yaliyozaa vurugu siku ya Uchaguzi wa Oktoba 29, mwaka jana.
Taarifa ya tume hiyo kuikabidhi ripoti yake, imetolewa jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Aprili 21, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Othman Chande, alipozungumza na waandishi wa habari.
Amesema jumla ya watu 63,603 wameifikia tume hiyo kutoa ushahidi wao kwa njia mbalimbali, ikiwemo kukutana ana kwa ana, kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na dodoso.
Jaji Chande amesema ripoti hiyo itakayotolewa inatarajiwa kuwekwa hadharani kwa sababu ya maslahi ya umma na kuwezesha watu waone uhalisi wa nini kilitokea.

Social Plugin