Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMANI NI HAZINA YA SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII, TUILINDE- RAIS SAMIA


Na Mwandishi wetu, Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa amani ni hazina ya shughuli zote za kiuchumi na kijamii, akibainisha kuwa bila ya amani hakuna kujenga kujenga uchumi wala shughuli yoyote ya kiuchumi inayoweza kufanyika kwenye jamii.

Mhe. Rais Samia amebainisha hayo leo Jumanne Aprili 21, 2026 Jijini Dar Es Salaam, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Mama na Baba Lishe, akirejea matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2026 na namna ambavyo wananchi walishindwa kufanya shughuli zao.

"Nawapongeza kwa kaulimbiu ya Kongamano hili isemayo 'Shiriki kulinda amani na mshikamano wa Taifa, amani ni hazina ya Mama na Baba lishe' mlishuhudia siku tatu zile hakukuwa na kuchezana, hakukuwa na harusi, hakuna mikusanyiko, hakuna chochote. Zilikuwa siku nzito kwahiyo kaulimbiu hii ina mashiko makubwa sana." Amesema Rais Samia.

Akiwaomba Watanzania kuendeleza amani na utulivu wa Tanzania, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa Watanzania, akiipongeza na kuishukuru sekta binafsi nchini kwa mchango wanaoendelea kuutoa katika ustawi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na namna ambavyo Umoja wa Mama lishe Tanzania unavyojijenga katika sura ya Muungano kwa kujumuisha wajasiriamali hao kutoka Bara na Zanzibar.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com