Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA WAICHAKAZA YANGA KOMBE LA MUUNGANO!!



Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kutwaa Kombe la Muungano baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, katika fainali iliyopigwa leo Aprili 29, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Selemani Mwalimu katika dakika ya 120 kwa mkwaju wa penalti, kufuatia Clatous Chama kuchezewa madhambi ndani ya eneo la hatari dakika ya 117.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulimalizika kwa sare tasa ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyomlazimu mwamuzi kuongeza dakika 30 za nyongeza (extra time) ili kupata mshindi wa fainali hiyo.

Kwa ushindi huo, Simba SC wanatwaa ubingwa huo na kujinyakulia Kombe pamoja na zawadi ya shilingi milioni 150, huku Yanga SC wakiridhika na nafasi ya pili na kupata shilingi milioni 100.

Hii ni mara ya saba kwa Simba SC kutwaa taji hilo, wakilingana na rekodi ya watani wao Yanga SC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com