
Ufafanuzi.
Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.
Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;
1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.
2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.
3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.
Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiani Duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.
Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Duniani ikiwemo Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Social Plugin