Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAJI CHANDE: SOTE TUNATAKA UWAJIBIKAJI, LAKINI WA HAKI



Na mwandishi wetu, Dar

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema tume inataka uwajibikaji wa haki kwa waliohusika na matukio ya vifo vya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 28,2026, Jaji Chande amesema tume imefanya kazi yake ya uchunguzi na ikatoa mapendekezo kwa kile kilichobainika iundwe tume ya kuchunguza ili hatua za kisheria zichukuliwe.

"Kwanza hakuna mtu yoyote aliyekuja mbele ya tume akasema kusiwepo na uwajibikaji sote tunakubaliana. Si jambo geni kila mmoja tunakubaliana kuwe na uwajibikaji na hakuna aliyesema hapana na kila mmoja ametaka uwajibikaji lakini tunachosema kuwe na uwajibikaji wa haki.

“Tulishauriwa na viongozi wakuu wa nchi tuliowaona kwamba anayestahili kuwajibika awajibishwe kwa mujibu wa sheria na asiyestahili kuwajibishwa asiwajibishwe.

"Wengine wakaenda mbali zaidi kwamba asitolewe mtu kafara kwenye kuwajibishana ,Ushauri huo tulipokea na ilibidi tusikilize pia maoni ya watu," amesema Jaji Chande.

Amesema hawaamini katika uwajibikaji wa rejareja ambao ni mtu kutiwa hatiani na kuachiwa huru kwa kukosekana ushaidi.

“Hivyo ushahidi wake unatakiwa na uzito unaojiotosheleza ili mahakama ichukue hatua stahiki,” amesisitiza Jaji Chande.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com