Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BEI YA DHAHABU YAENDELEA KUPANDA, YAFUNGUA AJIRA NA MAPATO



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Sekta ya Madini nchini imeendelea kudhihirisha ubora wake katika kuchangia uchumi wa Taifa baada ya kuongoza kwa kuvutia mtaji wa uwekezaji kutoka nje ya nchi (FDI), ambayo inachangia takribani robo tatu ya mtaji wote uliowekezwa katika sekta muhimu nchini.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2025, thamani ya mtaji wa uwekezaji katika Sekta ya Madini imeongezeka hadi kufikia dola za Marekani bilioni 9.79 kwa mwaka 2024, kutoka dola bilioni 9.15 za mwaka 2023 na dola bilioni 8.64 za mwaka 2022.

Akiwasilisha Bungeni Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa, mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali kwa wawekezaji yameendelea kuvutia wawekezaji wapya na kuwahamasisha waliopo kupanua miradi yao pamoja na kuwekeza zaidi kupitia faida wanazozipata

Waziri Mavunde amesema kuwa, katika kipindi cha mwezi Julai 2025 hadi Machi 2026 , bei ya dhahabu katika Soko la Dunia imepanda kwa kasi na kufikia wastani wa dola za Marekani 4,190.47 kwa wakia, ikilinganishwa na dola 2, 655.80 katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia.

Akielezea mwenendo wa biashara ya Madini ya Almasi Duniani imeendelea kushuka na kufikia wastani wa dola za Marekani 159.84 kwa karati, kutoka dola 168.95 kwa karati katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25 , sawa na upungufu wa asilimia 5.39.

Aidha, Waziri Mavunde amebainisha kuwa, kushuka huko kunachangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa almasi za viwandani( Synthetic diamonds) ambazo zimepunguza

uhitaji wa almasi asilia katika masoko makubwa duniani ikiwemo China na Marekani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com