Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BALOZI NYALANDU: TUIMARISHE MSHIKAMANO KULINDA AMANI YA TAIFA



Katika kipindi ambacho dunia inaangalia mwenendo wa usalama na utulivu wa mataifa, kauli ya serikali imeendelea kuweka msisitizo mkubwa juu ya jukumu lake la msingi la kulinda maisha na mali za wananchi.


Hili limebainishwa wazi na Mshauri wa Rais wa Diplomasia, Balozi Lazaro Nyalandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa.

Akiweka msimamo wa serikali bayana, Balozi Nyalandu alieleza kuwa kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaakisi dhamira ya dhati ya kuhakikisha kila mwananchi anahishi salama na kulindwa bila kujali changamoto zinazojitokeza.

Ripoti ya Tume ya Jaji Chande imekuwa nyenzo muhimu katika kuweka wazi ukweli ambao kwa muda ulikuwa ukizua maswali miongoni mwa wananchi, Kupitia uchunguzi wa kina, tume hiyo imeweka hadharani mambo muhimu, ikiwemo hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na hali hiyo, Hii ni ishara ya uwajibikaji na uwazi unaopaswa kupongezwa.

Kwa muktadha huu, ni muhimu kwa jamii kutambua tofauti kati ya haki ya kuandamana kwa amani na vitendo vya vurugu vinavyohatarisha usalama wa taifa. Wananchi wanapaswa kuwa macho, kushirikiana na vyombo vya dola, na kuepuka kushawishiwa kujiingiza katika matendo yanayoweza kuleta madhara makubwa.

Ulinzi wa taifa si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja wetu. Kwa kushirikiana, tunaweza kujenga jamii yenye amani, mshikamano, na maendeleo endelevu.

Ni wakati wa kusimama pamoja, kuilinda nchi yetu, na kuhakikisha kuwa mustakabali wa vizazi vijavyo unabaki salama na thabiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com