Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUMISHI WANAWAKE BANDARI YA TANGA WATOA MSAADA WA MASHINE YA KUWASAIDIA WATOTO WACHANGA KUPUMUA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA-BOMBO







Na Oscar Assenga,TANGA

Watumishi Wanawake Bandari ya Tanga imesheherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kwa kutoa msaada wa Mashine ya Kuwasaidia watoto wachanga kupumua na Oyxgen Flowmeter katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 5.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Afisa Rasimali Watu wa Bandari ya Tanga Bi. Sharifa Konshuma Nuhu alisema wamekuwa wakitumia siku hiyo kufanya matendo ya huduma kwa jamii zinazowazunguka na mwaka huu wameamua kwenda Bombo Hospitali kwa ajili ya kutoa msaada


Alisema kwamba msaada huo ni kuchangia nguvu zao kwa juhudi za Serikali kuhakikisha wanaboresha afya za watoto na raia wa nchi na wao walichagua kutoa mashine hizo kwa wodi ya watoto wachanga wanaozaliwa kutokana na changamoto mbalimbali na kutambua umuhimu wa watoto .


Alisema kwamba watoto ni Taifa la kesho ambalo linatakiwa lijengwe hivyo wanahitaji watoto wenye nguvu,watu wenye nguvu ambao wataleta mchango mkubwa kuhakikisha nchi inasonga mbele.


“Tulifika hapa tukafahamu mahitaji na Mkuu wa Idara ya Watoto wanachangamoto hizo za watoto hivyo tukaona tuwashike mkono bombo kutokana na Hospitali ya Rufaa ya Bombo ndio hospitali zote wagonjwa wanapewa rufaa kutoka wilayani kufika hapa kwa kiasi kidogo ambacho tumekifanya kitakuwa kimeongeza huduma”Alisema


Hata hivyo alisema kwamba vifaa vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5 waliona wachangie ili kuweza kufikisha malengo na wanajisikia furaha na faraja kutokana na furaha ya mama ambao wanapata watoto salama na huzuni kwa wale wanaowazaa wenye changamoto .


Awali akizungumza baada ya kupokea msaada huo ,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Abdi Msangi aliwashukuru kwa msaada huo ambao wameutoa kutokana na kufika wakati muafaka kutokana na uwepo wa upungufu mkubwa wa vifaa vya kuwahudumia watoto na watoto wachanga wenye matatizo ya upumuaji


Alisema hasa ukizingatia kumekuwa na ongezeko kubwa kwa watoto wanaozaliwa na wanaopewa rufaa kwenda kwenye hospitali hiyo kupata huduma hizo ambao wanakuwa na changamoto za kupumua kwa hiyo wanashukruu kwa msaada huo ambao utaendelea kuboresha huduma wanazotoa kwenye Hospitali hiyo.


Alisema huduma hizo zitaendelea kuboreshwa hasa katika idara ya watoto na watoto wachanga huku akiwahimiza wadau wengine waliopo Tanga na nje kuendelea kuwasapoti kwenye nyanja mbalimbali za utoaji huduma na hiyo itasaidia kuboresha huduma na kukava ile gepu.


Naye kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Mohamed Salehe alisema kwamba wanawashukuru TPA Tanga kwenda na kutembelela wodi ya watoto na kuwapelekea zawadi kati yao mashine ya Simpapu kuwawezesha hasa watoto waliozaliwa kabla ya siku zao (watoto ) kuweza kupumua.


Alisema na mashine ya Suction ambayo inasidia kuvuta katika njia ya hewa ikiwa kuna uchafu kwa mtoto na mashine nyengine ambazo ni msaada mkubwa kwenye wodi yao pamoja na hayo wameweza kutoa zawadi kwa wakina mama na watoto na wamefarijika kwa ujio wao na wameona hispitali yao imeweza kuonwa na uhitaji ni mkubwa.


Aidha alisema kwamba changamoto za hospitali hazikoesekana kutokana na hospitali ya mkoa wanapata watoto wengi wanaolazwa na kupelekea mahitaji waliokuwa nayo yanavuka uwezo hospitali walionao.


Aliongeza kwamba vifaa vimefika wakati muafaka kwa maana idadi ya watoto wanaolazwa inaongezeka kadri siku zinavyokwenda kuonekana umuhimu wa hiyo huduma kutokana nawali walipokuwa wakizaa watoto njiti walikuwa wanaona hawana uwezo wa kuweza kuishi.


“Lakini baada ya kuona huduma zipo watu wanaona umuhimu wa kuwapeleka Hospitali watoto kupata huduma huku akieleza hizo mashine zitakuwa msaada mkubwa na tunawaomba na wadau wengine waone umuhimu wa kujitokeza kuwasaidia kuokoa maisha na kuwasaidia “Alisema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com