Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, pamoja na Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni wa TFS Kanda ya Magharibi, wakiwa wameshikilia miche ya miti tayari kwa zoezi la upandaji katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga 'Shinyanga Girls Secondary School' wakati wa maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi, inayojumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Shinyanga, imeadhimisha Siku ya Misitu Duniani kwa kufanya kampeni ya upandaji miti, ambapo zaidi ya miti 350 imepandwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga 'Shinyanga Girls Secondary School'.
Maadhimisho haya yamefanyika leo Machi 20, 2026 kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi wa mazingira, kukuza uoto wa asili, na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa misitu katika maisha ya kila siku, sambamba na kupunguza ukataji miti hovyo na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akiongoza shughuli hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa shule hiyo pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kulinda mazingira.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia nishati safi ya kupikia na kuacha ukataji miti hovyo ili kulinda misitu kwa vizazi vijavyo.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa TFS Kanda ya Magharibi, Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni Kanda hiyo, Shadrack Msilu, amesema upandaji miti katika shule hiyo ni fursa ya kuhamasisha jamii kuchukua hatua za moja kwa moja katika uhifadhi wa mazingira.
“Kila mwaka hekta za misitu 406,900 hupotea kutokana na ukataji miti holela, na ndiyo maana tunatoa elimu kwa wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi na kuacha kuikata,” amesema Msilu.
Mwenyekiti wa Club ya Mazingira shuleni hapo, Kabula Bundala, amesem shule hiyo ilianzishwa mwaka 2023 na kuanza na mti mmoja tu wa asili ambapo kwa kushirikiana na TFS wilaya ya Shinyanga, sasa shule hiyo hivi sasa ina jumla ya miti 12,053, ikionyesha mafanikio makubwa katika juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Katika hatua nyingine, waandishi wa habari wamepata fursa ya kutembelea eneo la utalii wa picha lililopo katika Msitu wa Lubaga, ambapo walijionea vivutio mbalimbali vya asili vinavyoweza kutumika kukuza utalii wa ndani na kutangaza rasilimali za misitu.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani.

Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni wa TFS Kanda ya Magharibi akizungumza wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda hiyo ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani. 

Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni wa TFS Kanda ya Magharibi akizungumza wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda hiyo ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akipanda mti wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani kwa kupanda miti Shinyanga Girls Secondary School.

Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni Kanda ya Magharibi (TFS) Shadrack Msilu akipanda mti.
Afisa Misitu Mwandamizi na Mkuu wa Operesheni Kanda ya Magharibi (TFS) Shadrack Msilu akipanda mti.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Shinyanga Girls Nurah Kamuntu akipanda mti.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry, akipanda mti Shinyanga Girls Secondary School wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani.
Mkurugenzi wa Malunde Media (Malunde 1 Blog), Kadama Malunde, akiwa ameshikilia mti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga (Shinyanga Girls Secondary School) wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani.
Mkurugenzi wa Malunde Media (Malunde 1 blog) , Kadama Malunde, akipanda mti Shinyanga Girls Secondary School wakati Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi ikiadhimisha Siku ya Misitu Duniani.

Social Plugin