Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MJOMBA MATATANI KWA KUMPIGA NA KUMNING'INIZA MTOTO DIRISHAJI KWA KUUNGUZA MBOGA




Na mwandishi wetu, Tabora

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linamshikilia Joseph Mbalamwezi Francis Mkazi wa Mtaa wa Imalamakoe B, Wilayani Urambo, Mkoani Tabora kwa tuhuma za kumfanyia mtoto ukatili wa kufungwa kamba miguuni na mikononi na kisha kumning'iniza dirishani.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ameviambia Vyombo vya habari leo Jumatano Machi 04, 2026 kuwa tukio hilo lilitokea Machi 02, 2026 na mtoto aliyekuwa anafanyiwa ukatili huo ana umri wa miaka 10 na kwamba mtuhumiwa ni Mjomba wake ambaye walikuwa wakiishi pamoja.

"Sababu za kumfanyia ukatili huo wa kupigwa na kisha kuning'inizwa inadaiwa ni baada ya mtoto huyo kuunguza mboga (nyama) aliyokuwa anapika." Amesema Kamanda Misime.

Jeshi la Polisi pia limewashukuru waliotoa taarifa za tukio hilo na kufanikisha mtoto huyo kuokolewa na kwenda kupatiwa matibabu na mtuhumiwa kukamatwa, Polisi ikisisitiza ushirikiano zaidi katika kuwalinda na kuzuia vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com