Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ikikagua mradi wa uboreshaji wa barabara ya kutoka Nguzonane kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga inayojengwa kwa kiwango cha lami.Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo na kusisitiza umuhimu wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na huduma zinazotarajiwa.
Ziara hiyo imefanyika leo Machi 10, 2026 ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, ambapo kamati hiyo ilitembelea miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa standi mpya ya mabasi ya Mkoa wa Shinyanga, ujenzi wa Soko Kuu la Shinyanga pamoja na mradi wa uboreshaji wa barabara ya kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katika ziara hiyo, kamati ilianza kwa kutembelea Shule ya Msingi Bugayambelele, ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa shuleni hapo.
Baada ya hapo kamati hiyo ilikagua mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Mkoa wa Shinyanga unaoendelea katika Kata ya Kizumbi.

Wakati wa ukaguzi huo, kamati ilipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaofanya kazi za vibarua katika mradi huo.
Baadhi ya wafanyakazi hao walisema wanalipwa ujira mdogo ambao hauendani na viwango vinavyotakiwa kisheria, huku wakidai pia kucheleweshewa malipo yao kwa takribani mwezi mmoja.

Walisema licha ya kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato, bado malipo yao yanachelewa na kiasi wanachopewa hakiridhishi.
Akizungumza baada ya kusikiliza malalamiko hayo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe alisema kamati hiyo imezipokea changamoto hizo na kuahidi kuzifuatilia ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinazingatiwa kwa mujibu wa sheria.
Katika hatua nyingine, kamati hiyo ilitembelea mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga ambapo wafanyabiashara waliendelea kueleza kilio chao cha kutaka mradi huo ukamilike haraka ili waweze kurejea kufanya biashara zao.
Mwenyekiti wa soko hilo alisema wakati wafanyabiashara wanahamishwa kutoka eneo la soko waliambiwa ujenzi ungechukua miezi sita pekee, huku mafundi wakifanya kazi mchana na usiku. Hata hivyo hadi sasa takribani miaka minne imepita bila mradi huo kukamilika.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Salum Kitumbo, aliwaomba wafanyabiashara kuwa na subira huku akiwahakikishia kuwa hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa kushirikiana na wataalam ili kuhakikisha ujenzi wa soko hilo unakamilika kwa ubora na kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Makombe alisema chama hicho kitaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuona mradi huo unakamilika na wananchi wanaanza kunufaika nao.
Aidha, kamati hiyo pia ilikagua mradi wa uboreshaji wa barabara kutoka Nguzonane kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga unaojengwa kwa kiwango cha lami, lakini ikaeleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.
Wananchi pamoja na madiwani wa Kata ya Ndani, Mhe. Zamda Shaban, na Diwani wa Kata ya Masekelo, Mhe. Peter Koliba, walisema viongozi mbalimbali wa serikali wamewahi kutembelea mradi huo na kutoa maelekezo, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita pamoja na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenan Kihongosi.
Hata hivyo, walisema licha ya maelekezo hayo, mkandarasi hajachukua hatua madhubuti na mradi huo umesimama kwa zaidi ya wiki moja bila kazi kuendelea kufanyika.
Kwa mujibu wa viongozi hao, mradi huo una mkataba wa miezi 15 lakini hadi sasa baada ya miezi saba kupita umefikia takribani asilimia 14 tu ya utekelezaji, hali inayoonyesha kusuasua kwa ujenzi huo. Walisema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo kumwondoa mkandarasi endapo ataendelea kuchelewesha mradi huo.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti Makombe alisema kamati hiyo itaendelea kufuatilia kwa karibu ili kubaini changamoto zilizopo na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.
Katika ziara hiyo, kamati pia ilitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga Girls, ambapo ilikagua ujenzi wa bweni pamoja na miundombinu mingine ya shule hiyo. Viongozi wa kamati walitumia fursa hiyo kuishauri serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuweka uzio kuzunguka shule hiyo kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wanafunzi.
Kadhalika, kamati hiyo ilitembelea Soko la Mitumbani lililopo Kata ya Ngokolo na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara wa soko hilo.
Wafanyabiashara walisema baadhi ya miundombinu ya soko hilo si rafiki hasa wakati wa mvua ambapo maeneo mengi hujaa maji na kufanya mazingira ya biashara kuwa magumu.
Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu la chama hicho la kufuatilia miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazokusudiwa na serikali.
Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ikikagua maendeleo ya ujenzi wa standi mpya ya mabasi ya Mkoa wa Shinyanga inayojengwa katika Kata ya Kizumbi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, akizungumza.

Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Salum Kitumbo akizungumza baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa standi mpya ya mabasi.
Samwel Jackson katibu wa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza.

Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga alikataa kuzungumzia malalamiko ya vibarua wake.
Mmoja wa wananchi wanaofanya vibarua katika mradi wa ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga akieleza malalamiko yake.

Kamati hiyo ikiwa katika mradi wa ujenzi wa Soko kuu la Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, akizungumza baada ya kutembelea ujenzi wa soko kuu la Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Soko akieleza athari zilizopo.
Diwani wa Kata ya Masekelo Mhe. Peter Koliba
Diwani wa kata ya Ndani Mhe. Zamda Shaban

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, akitoa maelekezo baada ya kutembelea uboreshaji wa barabara ya Mwawaza.
Mkuu wa shule ya sekondari Shinyanga Girls Mwalimu Nurah Wilfred akisoma taarifa fupi ya shule hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akipokea taarifa ya shule hiyo.

Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ikikagua ujenzi wa bweni na miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga Girls.

Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ikitembelea Soko la Mitumbani lililopo Kata ya Ngokolo.

Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ikisikiliza changamoto za wafanyabiashara katika Soko la Mitumbani lililopo Kata ya Ngokolo.

Social Plugin