Kuna maumivu ambayo hayaonekani kwa macho, lakini yanachoma ndani kama moto wa polepole. Hayo ndiyo aliyopitia Juma, kijana wa miaka ishirini na nane kutoka Kayole, baada ya bodaboda yake kuibiwa alfajiri moja wakati ndiyo ilikuwa chanzo chake pekee cha riziki.
Juma hakuwa na kazi nyingine. Bodaboda ile aliinunua kwa mkopo wa chama cha vijana. Kila siku aliamka saa kumi alfajiri, akapiga kazi hadi jioni, akalipa marejesho kidogo kidogo. Alikuwa karibu kumaliza kulipa.

Social Plugin