
Katika kuadhimisha Wiki ya Maji mwaka 2026, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), imekutana na maafisa usafirishaji, maarufu kama Bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga na kuwapatia elimu kuhusiana na utunzaji wa miundombinu ya maji na kuwafanya mabalozi wa utoaji wa taarifa za uvujaji, uharibifu wa miundombinu ya maji na wizi wa maji.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 18 Machi 2026 kwenyea viwanja vya SHUWASA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Nsianeli Gerald, amesema Mamlaka hiyo imeona umuhimu wa kuwashirikisha bodaboda kutokana na urahisi wao wa kufika katika maeneo mbalimbali na kubaini uharibifu wa miundombinu au uvujaji.
Amesema pia bodaboda wanakutana na watu wengi hivyo ni rahisi kwa wao kufikisha elimu kwa watu wengine kuhusiana na masuala yanayohusu maji na utunzaji wa mazingira.
"Tunaomba kule mnakofika kupeleka wateja, huko barabarani mnaweza kukutana na mivujo",amesema.

















Social Plugin