Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WA HABARI NA WAHARIRI KUKUTANA IRINGA KATIKA KONGAMANO LA MISA TAN SUMMIT 2026


Kongamano la wadau wa habari, Wahariri na Waandishi wa habari l(Wanachama wa MISA Tan) la mwaka  Tan 2026 linaloandaliwa na MISA Tanzania linatarajiwa kufanyika Machi 17, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ambaye anatarajiwa kufungua rasmi mkutano huo utakaowakutanisha wadau mbalimbali wa habari, toka Serikalini, Sekta Binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Kongamano hilo linalojulikana kama MISA TAN Summit 2026 linalenga kujadili changamoto na fursa zilizopo katika tasnia ya habari pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya wahariri, waandishi wa habari na wadau wengine wa mawasiliano nchini.

Akizungumza kuhusu kongamano hilo, Mwenyekiti wa MISA TAN, Edwin Soko amesema kuwa mkutano huo utatoa jukwaa la kubadilishana uzoefu, kujadili maadili ya taaluma ya uandishi wa habari pamoja na kuangalia namna bora ya kutumia vyombo vya habari katika kuimarisha uwajibikaji na maendeleo ya jamii.

Soko amesema kuwa, kongamano hilo limeletwa Mkoa wa Iringa maksudi kwa kuwa MISA Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Mhe. Kheri James kwenye kuchapa kazi na kuleta maendeleo Mkoani humo hivyo uwepo wa waandishi wa hanari kwenye kongamano hilo utasaidia kutangaza maendeleo ya Mkoa wa Iringa.

Soko ameongeza kuwa MISA Tanzania itaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Rais Samia Suluhu ili kusukuma mbele maendeleo ya Taifa.

Pia Wahariri na wanachama wote wa MISA Tanzania watapata siku moja ya kufanya ziara kwenye vivutio mbalimbali vya Mkoa wa Iringa ikiwemo Hifadhi ya Ruaha iliyopo Mkoani humo.

Kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Iringa Imara Tutajenga kwa Umoja na Uwajibikaji”, ikiwa ni wito kwa wadau wa habari kushirikiana katika kulinda maadili ya taaluma na kuhakikisha habari zinazotolewa kwa umma zinachangia maendeleo ya taifa.


MISA Wadau Summit itaendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa kutangaza fursa za sehemu husika na kila Mwaka itakuwa inazunguka Mkoa mmoja baada ya Mwingine kama ilivyoanza Mwaka Jana ambapo ilifanyika Jijini Dodoma na sasa imafanyika Mkoani Iringa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com