
Kwa hatua hiyo ni dhahiri kuwa Serikali ya Awamu ya Sita haiko kwenye mwendo wa kusuasua, bali inakimbiza kuelekea mafanikio makubwa.
Miradi ilioyozinduliwa ni Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari.
Akizungumza Februari 11, 2026 wakati wa uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mtemere uliopo mkoani Pwani, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Dkt. Mwigulu amesema miradi hiyo ni kielelezo cha maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alibainisha kuwa ujenzi huo, uliotekelezwa kupitia mradi wa kimkakati wa kukuza utalii ukanda wa Kusini (REGROW), unalenga kubadilisha sura ya utalii nchini kwa vitendo.
Uzinduzi huo ni sehemu ya sifa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia; maneno kidogo, matendo zaidi.
Kwa hatua hizo inadhihirisha kama taifa kwamba Hatuendi mdogo mdogo, tunakimbiza ili kuhakikisha sekta ya utalii inachangia vilivyo katika pato la taifa.Vilevile, Serikali imenunua jumla ya mitambo mikubwa 18, malori 46, matrekta 7 na vifaa vingine mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza sekta hii ya uhifadhi na utalii.
Pamoja na uzinduzi huo Dkt. Mwigulu ametoa agizo kwa mamlaka husika kuhakikisha miundombinu hiyo inatunzwa kwa weledi ili iendane na thamani ya fedha zilizowekezwa. Aidha alisisitiza kuwa uwanja wa ndege wa Mtemere unapaswa kuwa kichocheo cha usafiri wa anga, akiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na mashirika ya ndege kama ATCL kuanzisha ruti za kimkakati zitakazounganisha Dar/Zanzibar na hifadhi za Nyerere, Mikumi, Ruaha hadi Songwe.
Awali, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia idadi ya watalii imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 149 ikiwa ni ongezeko la watalii 2,294,495 mwaka 2025 kutoka watalii 922, 692. “ongezeko hili limetokana na uwekezaji mkubwa na wakimkakati katika sekta ya uhifadhi na utalii”
Social Plugin