Na mwandishi wetu, Dar
Bwana Rashid Kengwa Rashid Mkazi wa Ilala Mkoani Dar Es Salaam amesema kukosekana kwa amani katika jamii kunakwamisha maendeleo na ustawi wa wananchi pamoja na kutatiza uhuru wa wananchi kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi, msisitizo akiutoa kwa kila mwananchi kuwajibika kuilinda na kukataa vitendo vyenye kuhatarisha amani na usalama wa Tanzania.
"Suala la amani ni jambo la kushukuru kwasababu lipo kwa kiasi kikubwa sana na pasingekuwa na amani hata hapa nisingezungumza nanyi, tungekuwa ni watu wa kujificha tu na tumshukuru Mungu sana kwa amani hii aliyoendelea kutupatia." Amesema Bw. Rashid.
Rashid ameeleza pia tofauti ya Tanzania na mataifa mengine yasiyokuwa na utulivu na amani, akisema kukosekana kwa amani kumesababisha madhila makubwa kwa watu wengi ikiwemo vifo, kuongezeka kwa umaskini pamoja na kukosekana kwa uhuru na hivyo kuua fursa za raia kujiendeleza kiuchumi pamoja na kuishi katika wasiwasi na hofu.

Social Plugin