
Siku hiyo haikuwahi kutoka kwenye kumbukumbu za maisha yake. Ilikuwa ni siku ya huzuni nzito, machozi yasiyokauka, na maumivu ya kumpoteza mtoto. Alijifungua mapacha wawili, lakini furaha ile iligeuka haraka kuwa kilio.
Madaktari walitangaza kwa masikitiko kuwa mmoja wa mapacha hao hakunusurika. Bila maswali mengi, bila muda wa kuhoji, waliambiwa mtoto amekufa. Kwa moyo uliojaa maumivu, familia ilifanya mazishi. Mtoto yule mdogo alizikwa, na maisha yakalazimika kuendelea.
Social Plugin