Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA - ETHIOPIA



Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi zake za Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Duniani – Global Partnership for Education (GPE) – pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Maji Kusini mwa Afrika – Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA), ameshiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.


Katika mkutano huo wa ngazi ya juu, Rais Mstaafu alipata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo mafupi na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, pia alikutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Nchi na Serikali waliopo madarakani, Wakuu wa Nchi Wastaafu wenzie pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika, wakijadiliana masuala ya maendeleo, elimu na rasilimali maji kwa mustakabali wa Bara la Afrika.

Ushiriki wake katika mkutano huo umeendeleza mchango wa Tanzania katika mijadala ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda na maendeleo endelevu.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com