Na Raymond Mushumbusi WMJJWM- Dodoma
Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma limeshirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika upandaji Miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Samia aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo kwa kupanda mti ikiwa na lengo la kulinda na kihifadhi mazingira.
Wakizungumza mara baada ya zoezi hilo Wazee hao qwamempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahiri na thabiti katika kuliongoza taifa kwa misingi ya amani na utulivu.
"Tunampongeza Rais Samia kwa hatua yake ya kuitumia Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kuhamua kupanda Miti ili kuleta hamasa kwa watanzania katika kuyapenda na kuyatunza mazingira" wamesema Wazee hao.
Akiongoza zoezi hilo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi Januari 27, 2026 amesema lengo ni kuenzi maono ya Rais Samia la kutunza mazingira yanayotuzunguka.
Naibu Waziri Mahundi amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha kiongozi maono, mbunifu wake na namna anavyojali maslahi ya Taifa.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Wizara imeshirikiana na kundi la Wazee kuwakilisha Makundi Maalum yanayosimamiwa na Wizara katika zoezi hilo ambalo lina lengo kulinda na kutunza mazingira.
Zoezi la upandaji Miti mbele ya Ofisi ya Waziri Mtumba Jijini Dodoma limehusisha Kundi la Wazee Mkoa wa Dodoma, Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo.



Social Plugin