Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIMU WAISHUKURU SERIKALI KWA KUTHAMINI UTENDAJI KAZI WAO


Waalimu wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuthamini utendaji Kazi wao unaoleta matokeo chanya ya ufaulishaji kwa wingi Wanafunzi.

Hayo yamejiri Leo Jumatatu 26 Januari 2026 kwenye tukio la kuwapongeza Waalimu wa Shule ya Msingi Nanditi iliyopo Kata ya Chikunja wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

"Sisi Waalimu tunaipongeza na kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyotujali Waalimu. Na kipekee tunakushukuru sana Gavana Shilatu kwa uamuzi wako kutopongeza sisi Waalimu kutokana na ufaulishaji wa Wanafunzi, haijawahi kutokea ila imetokea kwako Shilatu. Ubarikiwe sana", alisema Venance Matimbe Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nanditi.

Akizungumza kwenye tukio hilo Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye tukio hilo la kuwaita Waalimu na kupongeza kwa ufaulishaji kwa asilmia 100 Wanafunzi wote.

"Nimeona niwaite niwapongeze kwa kazi nzuri ya ufaulishaji na pia iwe Chachu muendelee kufanya  vizuri na kwa wengineo pia nao wafanye vizuri zaidi. Kiukweli Waalimu na Wanafunzi mmetutoa kimasomaso kwa matokeo mazuri kwa Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba na Darasa la Nne. Kwa mfano kwa Darasa la 7 mmefaulisha Wanafunzi wote. Haijawi tokea tangu Dunia iumbwe kwa Shule yenu, hongereni sana", alisema Shilatu.

Akizungumza kwa niaba ya Wazazi Mwanaharusi Miliani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule amewapongeza Waalimu kwa kusimamia vyema Taaluma hali inayoleta matokeo mazuri ya Watoto wetu kufaulu sana.

Pia Shilatu alipata fursa ya kuongea na Wanafunzi Darasa la 7, kukagua hali ya uripoti Wanafunzi na kujiridhisha juu ya upatikanaji wa Chakula Shuleni ambapo ameona Wanafunzi wote wakipata Chakula Shuleni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com