Na Bora Mustafa, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, ameutaka uongozi wa Jiji la Arusha kutumia mapato yake ya ndani kuboresha masoko ya machinga ya Ulezi na Machame ili yaweze kutumika kikamilifu na wafanyabiashara wadogo.
Mhe. Makalla amebainisha hayo Januari 30, 2026, jijini Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua masoko hayo.
Aidha, ameagiza wafanyabiashara wadogo kupewa nafasi ya kufanya biashara katika masoko makubwa ya Kilombero na Mrombo mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake, unaotarajiwa kukamilika baadaye mwaka huu.
Kwa upande wa wafanyabiashara wamewasilisha changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, ikiwemo mazingira yasiyo rafiki kwa ajili ya kufanya biashara zao.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Arusha, Bi. Amina Njoka, alimshukuru Mhe. Makalla kwa ziara yake na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wadogo wapo tayari kulipa kodi na kushirikiana na Serikali wakati wote, mradi wapatiwe maeneo bora na rafiki ya kuendesha shughuli zao za kibiashara.





Social Plugin