
Mwandishi wetu,maipac.
maipacarusha@gmail.com
Mamia ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro wenye changamoto za kiafya leo wamejitokeza kupata elimu, kufanyiwa vipimo na baadhi kuanza kupata tiba bila kumeza vidonge wala kuchomwa sindano.
Tiba hiyo,imetolewa katika eneo la Bomang'om²be na kuwavutia watu wengi kutoka wilaya za mkoa huo na maeneo ya jirani.
Tiba hiyo, maarufu kama life Wive kutoka nchini Uingereza inatolewa kupitia Phototherapy na imekuwa ikivutia mamilioni ya watu duniani.
Akizungumza baada ya kufanyiwa vipimo,Mary Meena mkazi wa Boma anasema amekuwa akisumbuliwa na moyo na labla kufika kwa wataalam.hao wa vipimo na tiba bila kumeza dawa alikuwa tayari amepima hospitali.
"Nimekuja hapa nimepimwa kwa mfumo wao ambao unatumia kompyuta na changamoto zote ambazo zilionekana hospitali pia nao wameziona ikiwepo kusumbuliwa na moyo na baadhi ya mirija kupanuka",amesema.
Amesema ameridhishwa na utaalam huo wa kisasa wa kufanya vipimo ambavyo majibu yake yanafanana asilimia 100 na hospitali lakini kwa gharama ndogo.
Hata hivyo anasema changamoto ambayo anaiona kwa tiba hii ya kisasa ni gharama kubwa ya dawa hasa kwa familia duni.
"Wanapima vizuri,wanaona tatizo na wanakupa ushauri mzuri sana ila naona mimi dawa zao ndio kidogo zipo juu kama ambavyo unajua dawa za Ulaya bei yao ipo juu",amesema.
Lucy Mollel amesema baada ya kupewa elimu anaona matibabu ya lifewave ni mkombozi wa afya kwa sasa kwani kuna magonjwa mengi yanajitokeza sasa kutokana na matumizi makubwa ya dawa.
"Siku hizi dawa zimekuwa nyingi na nyingi zinasumu ambazo zinaathiri afya hivyo kupata tiba bila ya kumeza dawa wala sindano ni mapinduzi ya afya" ,amesema.
Akizungumza kabla ya kutoa vipimo na tiba Mtendaji mkuu wa Taasisi ya afya ya Life Wave Tanzania, Dkt. Sam Magesa anasema tiba hiyo ni rafiki kwa afya ya binadamu na ni mkombozi kwa wagonjwa.
Dkt. Magesa amesema vipimo na tiba zao zimethibitihwa na Mamlaka ya Tiba na Dawa(TFDA) lakini pia na mashirika makubwa ya Afya duniani.
" Wagonjwa wengi hivi sasa wana changamoto ambazo zimechangiwa pia na matumizi ya dawa kwa muda mrefu mfano kwa wagonjwa wa Moyo,Kisukari,Kansa na mengine na hivyo magonjwa yamekuwa sugu ",amesema.
Amesema teknolojia ya tiba ya phototherapy ni suluhu ya magonjwa mengi ambayo yamekuwa yakiwapata watu.
Dkt. Magesa anasema baada ya vipimo wanatoa dawa ya ALAVUDA ambayo inatibu magonjwa ya ngozi,wanatoa tiba Glutathione kuondoa sumu mwilini ,tumbo kujaa gesi na kusafisha figo.
"Pia tuna Ice Wave inatibu maumivu ya kichwa na misuri,X39 inatibu cancer,nguvu za kiume,ganzi,ipo X49 inatibu moyo na kuimarisha mifupa na kuongeza madini na nyingine nyingi" amesema.
Anasema tiba hii ya kisasa inatolewa na dawa kutoka Uingereza na Life Wave Tanzania pekee ndio wanatoa huduma hiyo.
Kwa upande wake Profesa Suleiman Mwenda akizungumzia tiba hizo amewataka watanzania kujali afya zao kabla ya jambo lolote.
"Afya bora ndio kila kitu kwa binaadamu hivyo nashauri tujenge tabia ya kupima afya,kupata matibabu na tiba za Life wave ndio suluhisho kwa sasa",amesema.
Profesa Mwenda amesema kwa mkoa wa Arusha pia tiba hiyo itafanyika na tayari kuna maombi ya mamia ya watu.
Anasema.l pia dawa za magonjwa mbalimbali zitatolewa na kuuzwa na akawataka wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza kupimwa na kupata tiba.
Kwa maelezo kamili ya upatikanaji wa tiba unaweza pia kupiga simu namba 0686873440











Social Plugin