Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YAITAKA SERIKALI KUIMARISHA USALAMA NA AFYAKATIKA SEKTA ISIYO RASMI NCHINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Chakoma, akifuatilia taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF iliyowasilishwa mbele ya Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu.

*****************

Na Mwandishi Wetu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kupitiaWakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kupanua wigo wa usimamizi wamasuala ya usalama na afya ili kuifikia sekta isiyo rasmi ambayo inakabiliwa nachangamoto nyingi zaidi za usalama na afya mahali pa kazi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo yaJamii, Mhe. Hawa Chakoma, wakati akihitimisha kikao baina ya Kamati hiyo na Ofisi yaWaziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) ambacho kilikuwa ni maalum kwa ajili yakupokea taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF BungeniJijini Dodoma leo (Januari 19, 2025).

Mheshimiwa Chakoma ameipongeza Taasisi ya OSHA kwa kazi nzuri ya kuimarishaafya na usalama wa wafanyakazi nchini kupitia miongozo na ushauri unaotolewa nawataalam wa OSHA wanapotembelea na kufanya ukaguzi wa mifumo ya usalama naafya katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini.

Amesisitiza umuhimu wa OSHA kuweka utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wamaboresho ambayo yamekuwa yakitolewa kupitia kaguzi zao ili kuhakikisha kwambawaajiri wanayafanyia kazi ipasavyo.

“Sisi kama Kamati licha ya kuwapongeza kwa kazi yao, tumewataka kuweka utaratibuendelevu wa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwasababu kuna taarifa ya uwepowa waajiri ambao wamekuwa wakizingatia matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya Mhali pa kazi pindi wanapotembelewa na wakaguzi wa OSHA. Kinyume na hapokunakuwa na upuuziaji wa kanuni na taratibu za kuwalinda wafanyakazi katika shughuliza uzalishaji,” ameeleza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo yaJamii.

Aidha, Kamati imeishauri serikali kuangalia namna bora ya kuijumuisha sekta isiyorasmi katika mfumo rasmi wa usimamizi taratibu za usalama na afya ili kulindanguvukazi kubwa iliyojiajiri katika sekta isiyo rasmi zikiwemo sekta ya usafirishaji naujenzi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la IlemelaMwanza, Mhe. Kafiti William Kafiti amesema kupitia kikao hicho Kamati imepata fursaya kuelewa kwa undani namna ambavyo Taasisi hizo muhimu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) zinavyotekeleza majukumu yake ya msingi jamboambalo litaleta tija katika utekelezaji wa jukumu la msingi la Kamati hiyo la kuishairiOfisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na Taasisi chini yake.

Akiwasilisha taarifa kuhusu muundo wa majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Waziri mwenyedhamana ya Masuala ya Kazi, Mhe. Deus Sangu, ambaye aliambatana na MtendajiMkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na watendaji wengine wa Ofisi yake, ameielezaKamati hiyo umuhimu wa majukumu ya Taasisi hizo mbili katika kuchochea maendeleona kuleta ustawi wa wafanyakazi na waajiri nchini.

OSHA ni miongoni mwa Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusianoyenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 inayoweka msingi wa kitaifa wa usimamizi wa masuala yausalama na afya katika shughuli zote za kiuchumi ili kulinda nguvukazi na uwekezajinchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, akiwasilisha taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF mbeleya Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma leo (Januari 19,2026).

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii baada yakupokea taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF. Taarifahiyo iliwasilishwa mbele ya Kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu.

Baadhi ya wajumbe na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) wakiwa katika kikao cha Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ambacho kilikuwa nimahsusi kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), kuwasilisha taarifakuhusu muundo na majukumu ya Taasisi za OSHA na WCF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com