Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza Halmashauri zote Nchini Majiji kutochukuwa bidhaa halali za Wananchi ambao ni wafanyabiashara wadogo wanaojitafutia riziki zao Barabarani kulingana na mitaji yao hata kama wakikutwa na makosa ushughulikiwe utaratibu tu! na sio kuua mitaji yao midogo
"Huu utaratibu wa kuchukua bidhaa haukubaliki wafautilieni waliochukuwa bidhaa na kama hazipo hao ni wezi kama wezi wengine tusicheze na mitaji ya watu hatutapiga vita umasikini kama hatutaheshimu mitaji ya watu " Waziri Mkuu
Aidha ametumia jukwaa hilo kuwaambia kutangaza Ziara ya majiji yote Nchini kuangazia changamoto za wafanyabiashara hao na kuendelea kuacha utaratibu huo hapo hapo amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni mtu wa haki hivyo watendaji wasimuangushe

Social Plugin