
Mtazamo huo unaungwa mkono na Amina Jamal, ambaye anaeleza kuwa amani inapodumishwa, fursa za kiuchumi huongezeka na taifa hupiga hatua kwa kasi kubwa.
Amina anahimiza kila Mtanzania kuepuka vurugu na migawanyiko, akisisitiza kuwa ulinzi wa amani ni wajibu wa kila mmoja kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Aliongeza kuwa ni muhimu kujenga tabia ya kuheshimiana na kusikilizana ili kutatua tofauti kupitia mazungumzo badala ya mizozo.
Licha ya kuwepo kwa changamoto za kisiasa, baadhi ya vijana wameeleza kuwa mzalendo wa kweli hupimwa kwa vitendo na si maneno pekee. Wamesisitiza kuwa kwa kuchagua utulivu badala ya kelele za chuki na propaganda, wamethibitisha kuwa nguzo ya amani ya taifa imara.
Aidha vijana nchini wametakiwa kujiamini na kujitokeza kwa wingi katika kuwania fursa zilizopo nchini kwa kuhakikisha kwamba amani inaendelea kuwepo ili katika mazingira ya sasa ya ushindani na ukuaji wa uchumi, kuwepo na mazingira rafiki yatakayowafanya vijana kuonyesha vipaji vyao na uwezo wao katika ubunifu, utekelezaji, usimamizi na uongozi.
Social Plugin