Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MHITA AHIMIZA UWAJIBIKAJI,UPENDO NA MSHIKAMANO KISHAPU


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akizungumza katika kikao maalum kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Disemba 18,2025

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amewataka madiwani pamoja na menejimenti ya Halmashauri kudumisha umoja, upendo na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao, akisisitiza kuwa mshikamano huo ndio msingi wa kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na endelevu.
Mhe. Mhita ametoa wito huo Desemba 18, 2025, wakati akizungumza katika kikao maalum kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa amesema madiwani wote wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kwa nguvu zote kwa maslahi ya wananchi waliowachagua, huku akisisitiza umuhimu wa kutatua changamoto na kero za wananchi kwa haraka.

“Madiwani mna dhamana kubwa kutoka kwa wananchi. Ni wajibu wenu kufanya kazi kwa weledi, umoja na upendo ili kujenga Halmashauri imara na yenye maendeleo,” amesema Mhe. Mhita.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwalinda viongozi wote, wakiwemo madiwani, katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao bila kuathiriwa na nia ovu au fitina kutoka kwa baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa.

Mhe. Mhita pia amewataka madiwani wa viti maalum kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia makundi maalum katika jamii, huku akiwahimiza madiwani wa Kata kutoa ushirikiano wa dhati badala ya kuibua migogoro isiyo na tija.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza katika kikao maalum cha Mkuu wa mkoa huo Mhe. Mboni Mhita kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Disemba 18,2025

Aidha, Mhita amehimiza ushirikiano wa karibu kati ya madiwani, Mbunge na uongozi wa Halmashauri, akibainisha kuwa mshikamano huo ni nguzo muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo.

Akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti yake, Mhe. Mboni Mhita amesisitiza usimamizi thabiti na utekelezaji wenye tija wa miradi ya maendeleo, ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaokusudiwa.

Ameagiza kuendelea kuibua vyanzo vipya vya mapato ya ndani, sambamba na kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha za umma, akisisitiza nidhamu ya matumizi na uwajibikaji wa fedha

Mhe. Mhita amesisitiza umuhimu wa lugha nzuri, staha na heshima kwa wananchi wakati wa utoaji wa huduma, akieleza kuwa wananchi wanastahili kuhudumiwa kwa utu na haki.

"Pia nipende kuwapongeza watumishi wote mnaofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yenu na kwa wanaolalamikiwa mara kwa mara na wananchi nitoe onyo kwenu ni lazima mbadilike na pale inapobidi Mkurugrenzi hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma"ameongeza.Katibu tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza katika kikao maalum cha Mkuu wa mkoa huo Mhe. Mboni Mhita kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Disemba 18,2025

Katika kuimarisha demokrasia na ushirikishwaji wa wananchi, Mkuu wa Mkoa ameagiza kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa wingi, isiyo ya kusoma taarifa tu bali kusikiliza, kujadili na kutatua kero za wananchi moja kwa moja.

Akizungumza mara baada ya maelekezo ya Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Josephat Limbe kwa niaba ya Baraza la Madiwani, amesema wamepokea na kuyakubali maelekezo yote na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na uwajibikaji mkubwa, ili kuyatafsiri maelekezo hayo kuwa maendeleo halisi yanayogusa maisha ya wananchi. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza katika kikao maalum cha Mkuu wa mkoa huo Mhe. Mboni Mhita kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Disemba 18,2025

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri Emmanuel Johnson mbali na kumshukuru Mkuu huyo kwa ziara yenye mwelekeo mpya wa Halmashauri hiyo, amesema yeye na menejimenti wataendelea kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote kwa uadilifu, uwazi na uwajibikaji, akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuwaletea wananchi huduma bora na maendeleo endelevu.

“Menejimenti kwa ujumla wake tuataendelea kusimamia na kutekeleza maelekezo yote uliyoyatoa kwa uadilifu mkubwa, kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa thamani ya fedha na kwa maslahi mapana ya wananchi,” amesema Mkurugenzi.

Ameeleza kuwa Halmashauri itaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa miradi, ukusanyaji wa mapato ya ndani, pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza katika kikao maalum cha Mkuu wa mkoa huo Mhe. Mboni Mhita kilichowakutanisha madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri na menejimenti na wakuu wa Taasisi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Disemba 18,2025































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com