
Mh. Mbunge wa Jimbo la Bukoba Johnston Johansen Mutasingwa akizungumza na waandishi wa habari

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Mh Acton Jasson Lwankomezi akizungumza na waandishi wa habari
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera Mh.Jonston Johansen Mutasingwa amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuandika mambo yanayosaidia jamii lakini pia ambayo yatailinda jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari katika chakula cha mchana leo Desemba 5,2025 katika ukumbi wa St. Teresa uliopo Manispaa ya Bukoba alichowaandalia waandishi wa habari kwa kuwashukuru kwa kazi waliyoifanya wakati wa kampeni Mh. Mutasingwa amesema kuwa waandishi wa habari pia ni wasimamizi wa miradi inayotekelezwa kwa kuandika habari za mwendelezo kwa kila hatua ya miradi inayotekelezwa.
Mh. Mutasingwa ameongeza kwa kusema kuwa kalamu ya mwandishi wa habari inaweza kusababisha upepo kuwa mzuri ama hata kuwa mbaya hivyo amewataka kuwa makini na taarifa wanazozitoa kwa kulinda amani ya nchi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba amesema kuwa lengo ilikuwa kukutana na kula chakula pamoja na kufahamiana huku akiongeza kuwa nguvu ya habari ni kubwa kwa kuwataka kushirikiana katika kuhakikisha wanatumia kalamu zao kwa usahihi.






Social Plugin