Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda, amefungua rasmi semina elekezi kwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama leo Desemba 29, 2025, mafunzo yatakayodumu kwa siku tatu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, DC Nkinda amewataka madiwani kutumia nafasi walizopewa kuacha alama chanya itakayokumbukwa na vizazi vyao, akisisitiza kuwa wananchi wa Manispaa ya Kahama wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji uamuzi na hatua za haraka kutoka kwa viongozi wao.
“Tumieni nafasi zenu kutatua changamoto za wananchi na kuacha alama itakayokumbukwa na vizazi vyenu,” amesema DC Nkinda.
Aidha, DC Nkinda amenukuu maandiko matakatifu kutoka katika Biblia, Mhubiri 9:10, akiwahimiza madiwani kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe,” imenukuliwa sehemu ya maandiko hayo.
Kwa upande wa madiwani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama, Mhe. Mataluma Kaniki, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea uwezo madiwani ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya serikali.
Akielezea maudhui ya mafunzo hayo, Afisa Tawala Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Bw. Mashaka Makuka, amesema mafunzo yatahusisha mada mbalimbali zikiwemo majukumu na mipaka ya diwani, uhusiano kati ya madiwani na wataalamu wa halmashauri, usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo pamoja na maadili na uwajibikaji wa viongozi wa kuchaguliwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Bw. Masudi Kibetu, amesema mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, kwa lengo la kuwajengea uwezo madiwani, hasa ikizingatiwa kuwa kwa asilimia kubwa madiwani wa Manispaa ya Kahama ni wapya.
Amesema kutoa mafunzo mapema kabla ya kuanza kwa vikao vya Baraza la Madiwani kutawasaidia madiwani










Social Plugin