
Dar es Salaam.
Amani siyo maneno ni kazi. Vijana tukisimama pamoja, Tanzania inang'aa zaidi! Kaulimbiu hii imepata nguvu mpya baada ya Kampuni ya Meta, wamiliki wa majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii, kuchukua hatua madhubuti ya kuzifunga akaunti za watu wawili maarufu kwa uchochezi na uvunjifu wa amani nchini Tanzania: Mange Kimambi na Maria Sarungi Tsehai.
Hatua hii imepokelewa kwa shangwe na Watanzania wanaopenda amani, kwani inaonekana kama ulinzi wa moja kwa moja dhidi ya mipango ovu iliyokuwa ikipangwa kupitia majukwaa hayo.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usalama na jamii, akaunti hizi zilikuwa zimegeuzwa kuwa "ghala la fitina" na "kiwanda cha chuki". Walibainisha kuwa badala ya kutumika kwa mawasiliano ya kujenga, wamiliki wake walizitumia kama silaha za kisiasa zenye malengo ya kueneza uvumi na habari za uongo,zisizo na uthibitisho;Uchochezi wa kuingia mitaani wakihimiza umma kuingia mitaani bila sababu za msingi na kupora huku wakishirikiana na vikundi vya nje na mashirika yenye ajenda za siri zinazolenga kuvuruga uchumi na amani, wakiwa na silaha nyingine ya matumizi ya lugha chafu huku wakitukana viongozi wa taifa na taasisi za dola bila kuheshimu sheria.
Kufungwa kwa akaunti hizi hakuna maana ya "uminyaji wa uhuru wa kujieleza" bali ni hatua ya kuwawajibisha wale waliovuka mipaka ya uhuru na kuingia kwenye uhalifu wa moja kwa moja kama uchochezi, uenezi wa chuki na mipango ya kigaidi ya kisiasa. Uhuru wa kweli huja pamoja na wajibu wa kulinda amani na umoja wa Taifa.
Social Plugin