Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU MKUU RUWA’ICHI: KARDINALI PENGO ANAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA KIAFYA



Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa’ichi, amesema hali ya afya ya Kardinali Policarp Pengo, siyo nzuri kutokana na changamoto za kiafya zinazomkabili.

Taarifa ya Askofu Ruwa’ichi imetolewa leo tarehe 24 Desemba 2025 imetoa wito kwa Wakatoliki kumwombea Kardinali Pengo.

“Mzee wetu mpendwa Kardinali Policarp Pengo anakabiliwa na changamoto za kiafya. Zimefanyika jitihada za kumsaidia kimatibabu hapa kwetu. Hata hivyo, imeonekana kwamba upo uhitaji wa kumpeleka nje ya nchi ili apate matibabu ya uhakika zaidi.

“Kwa hiyo, mipango imefanyika ili akatibiwe nchini India. Tunatarajia kwamba ataondoka hivi karibuni kwa lengo la kupata matibabu hayo. Ninawaalika nyote tuungane kumsindikiza kwa sala na matashi mema,” amesema Askofu Ruwa'ichi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com