Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WAKUMBUSHWA MSINGI WA MAISHA YA KUTOPIGA CHUKU

Imeelezwa kuwa siri ya maisha ya Mtanzania imejengwa katika utamaduni wa kuvumiliana, jambo ambalo linawekwa hatarini na watu wanaochochea vurugu na uhasama. Watanzania wameaswa kulinda maisha yao ya kila siku kwa kuepuka kabisa chokochoko zinazoletwa na watu wenye maslahi binafsi.

Kauli hizo zimetolewa na watu mbalimbali mitandaoni  wakihimiza amanbi na kudharaui mipango ya wachochezi ya Desemba 25 . Mwananchi  mmoja katika mtandao amesisitiza umuhimu wa kuacha kabisa kujenga uhasama na kuvuruga maisha ya watu wa kawaida,akisihi wanaohubiri chuki na ugomvi washindwe na wananchi wasonge mbele katika maiksha yao ya kujenga taifa.

Ujumbe huu unaungwa mkono na sauti za wananchi wa kawaida, wakiwemo akina mama, ambao wanasema maisha yao yanategemea kuweka maisha yao ya siku kwa siku mbele ya mifarakano. Ni muhimu kwa Watanzania kujitambua kwamba amani huanza na mimi; mimi ndiye mlinzi wa amani yangu. Kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa vitendo na kauli zake na kuwa mzalendo wa kweli.

Uzalendo wa kweli nchini Tanzania, wanasema wachambuzi wa mambo, unapimwa kwa uwezo wa wananchi, hususan vijana, kuachana na tabia ya utegemezi wa misaada na badala yake kufanya kazi kwa bidii. Huu ndio ujumbe mkuu unaotolewa kwa kizazi cha sasa, kikiambiwa kuachana na vurugu na kuangalia mustakabali.

Inasisistizwa kuwa mustakabali wa nchi unategemea jinsi vijana watakavyofanya kazi kwa bidii na kuachana na tabia ya utegemezi wa misaada. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com