Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUMEPATA JUKWAA LA KUSHUGHULIKIA MASUALA YETU – FAUSTINE




Na Mwandishi wetu, Dar

Dar es Salaam – Uundwaji wa Wizara ya Maendeleo ya Vijana umeendelea kuibua matumaini mapya miongoni mwa vijana nchini, hususan wale ambao kwa muda mrefu hawakuwahi kupata mahali pa kuelekeza maoni na changamoto zao.

Akizungumza leo Alhamisi, Novemba 20, 2025, mkazi wa Ilala, Denis Faustine, amesema kuanzishwa kwa wizara hiyo ni hatua yenye manufaa makubwa kwa mustakabali wa vijana, kwani sasa mawazo yao yatafika kwenye mahali husika kwa urahisi zaidi.

 “Tunashukuru sana kwa hii Wizara ya Vijana iliyoundwa. Tunaona hata sisi sasa tutafikiwa, kwa sababu kuna wakati mawazo yetu tulikosa hata pa kuyapeleka. Kwa ujio wa Wizara hii ya Maendeleo ya Vijana naamini tutaitumia kuwasilisha mawazo na maoni yetu,” alisema Faustine.

Ameongeza kuwa wizara hiyo mpya inaleta dira mpya ya ushirikishwaji, uwazi na ufuatiliaji wa masuala yanayowagusa vijana ikiwemo ajira, ubunifu, ujasiriamali na elimu ya stadi za maisha.

Wachambuzi wa masuala ya jamii wanaeleza kuwa hatua hiyo ya Serikali inatarajiwa kuongeza uratibu wa programu za vijana na kuhakikisha kwamba maoni yanayotolewa yanatumika katika kupanga sera na mikakati yenye tija kwa taifa.

Central Blog itaendelea kufuatilia maendeleo ya Wizara hii mpya pamoja na maoni ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com