Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSIGWA AZUNGUMZIA MAKALA YA CNN, ASEMA UHAKIKI WA MAUDHUI YAKE BADO UNAENDELEA




Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa wito kwa Chombo cha habari cha CNN kutokana na makala waliyoichapisha kuhusu yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Nchini Tanzania Wito huo umekitaka chombo hiko kujiepusha kutoa Taarifa za Upande mmoja na kuchochea chuki

Wito umewasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa leo Novemba 23.2025 Jijini Dar es salaam alipokuwa katika Mkutano wake na Waandishi Habari

"Sio kweli kwamba CNN ilipata ugumu kupata upande wa Serikali inashangaza ,Serikali inatoa wito kwa CCN kujiepusha kutoa Taarifa kama zile najua Mwandishi hakuwa Tanzania ametumia video zilizopigwa na simu na amekwenda kuandaa makala ya upande mmoja " Gerson Msigwa

Ameendelea kuwa ,Ninaposema hivi Sishabiki vifo vilivyotokea lakini kwanini Mwandishi wa Habari ukachochee kuendelea kuwaumiza Wananchi mimi nimekwenda shule ile ni unprofessional na hairuhusiwi kusambaza habari mbaya kama zile Tume imeundwa itakuja na ripoti Serikali itachukuwa hatua " Msigwa

Pia amewataka CNN waje upande wa Serikali wasikilize na wachapishe mauldhui yenye ukweli waache kulalia upande mmoja sio sawa

Aidha wakati huohuo amewaomba Watanzania watambue kuwa Nchi yao iko salama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameunda Tume kwaajili ya matukio ya Oktoba 29 na matokea yatatolewa .



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com