TAARIFA KWA UMMA
Kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa leo jijini Dodoma, kuanzia kesho Jumanne tarehe 4 Novemba 2025, wananchi wote nchini wanajulishwa kurejea kwenye shughuli zao za kila siku za kiuchumi na kijamii.
Aidha, wananchi wanaaswa kuendelea kuzingatia tahadhari na miongozo ya kiusalama kadri itakavyokuwa inatolewa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao.
Imetolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi
3 Novemba 2025

Social Plugin