Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHULE YA ST. FRANCIS OF ASSIS YAFANYA MAHAFALI YA 11 KIDATO CHA NNE..YAJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA ELIMU

Jackson Mwakisu Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari ya St.Francis of Assis iliyopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Na Stella Herman,Shinyanga

Wazazi na walezi wametakiwa kuendelea kusimamia maadili na nidhamu kwa watoto wao ili kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye wenye uzalendo ikiwa ni pamoja na kuwaepusha na makundi maovu ambayo yanaweza kuharibu ndoto zao na kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yameelezwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jackson Mwakisu wakati akizungumza kwenye mahafali ya 11 ya kidato cha nne shule ya Sekondari St. Francis of Assis iliyopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambapo amesema vijana ni kundi ambalo linatakiwa kusimamiwa na kujengewa hofu ya mungu.

Amewataka wahitimu kuendelea kuwa na maadili mema kama walivyofundishwa walipokuwa shuleni ili kuwa na Jamii yenye maadili na kuandaa viongozi wenye uzalendo ,huku akiwatahadharisha kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujiepusha na mambo ambayo yanakiuka maadili.

“Vijana wengi wanaharibika kupitia utandawazi nawaomba sana endelee kuwa na nidhamu kama mlivyolelewa hapa shuleni mtakaporudi kwenye Jamii huko mtaani mtakumbana na mambo mengi kuweni makini na mkajiepushe na makundi yasiyozingatia maadili”,amesema Mwakisu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari St. Francis of Assis Shauri Maduhu amesema wanafunzi wanawajenga wanafunzi kwa kuwafundisha ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao ikiwa ni pamoja na kuwajenga kiroho.

Amesema shule hiyo inamiundombinu mizuri ambayo inawawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri yenye utulivu na kuwawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao,ambapo amewaomba wazazi na walezi waendelee kuwaamini na kupeleka watoto wao kusoma.
Makamu Mkuu wa Shule ya St. Francis of Assis Shauri Maduhu akisoma taarifa ya shule hiyo wakati wa mahafali ya 11 ya shule hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com