Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Oktoba 29, 2025, amejitokeza kupiga kura katika kituo cha Kijiji cha Chamwino, mkoani Dodoma, wakati wa zoezi la Uchaguzi Mkuu linaloendelea kote nchini.
Dkt. Samia alipowasili kituoni hapo mapema asubuhi, alijiunga na wananchi wengine kwenye mstari wa foleni akisubiri zamu yake kupiga kura tukio lililopokelewa kwa hisia kubwa za furaha na hamasa kutoka kwa wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Baada ya kupiga kura, Dkt. Samia amewataka Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya Kikatiba kwa utulivu, akisisitiza kuwa amani na mshikamano ni msingi wa maendeleo ya taifa.

Social Plugin