Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka wanawake wa Wilaya ya Tanganyika kujibu upotoshaji mitandaoni unaojaribu kuvuruga amani na mshikamano wa nchi, kwa kura ifikapo oktoba 29.
Akizungumza baada ya kuwasili wilaya Tanganyika leo tarehe 10 Oktoba 2025, ikiwa ni muendelezo wa kampeni amesema watu hao hawapaswi kujibiwa kwa maneno bali ni kwa kuipa ushindi CCM ili kuendelea kubaki madarakani.
Katika mkutano huo pia alimuombea kura za ndio mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja, kumnadi mgombea wa ubunge Ndg.Moshi Selemani Kakoso, na Wagombea nafasi ya Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Tanganyika.

Social Plugin