Na mwandishi wetu, DAR
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Pius Chatanda (MCC), ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini Dar es Salaam, amekutana leo Oktoba 16, 2025 na Maafisa Usafirishaji (Boda Boda) wa Kata ya Kinyerezi, Jimbo la Segerea, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Chatanda aliwahimiza vijana wa bodaboda kutokubali kupotoshwa na baadhi ya maudhui machafu yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na wanasiasa wa upinzani wasio na nia njema na Taifa.
Amesema ni muhimu kwa vijana hao kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano waliouonesha, sambamba na kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kupiga kura ya “NDIYO” kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, amewataka pia kumpigia kura ya ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, Bi. Bonnah Kamoli, pamoja na Madiwani wote wa CCM katika kata zote za Jimbo hilo.
Vijana wa bodaboda kwa upande wao wameahidi kuendelea kuwa mabalozi wa amani na maendeleo, wakisema wanatambua kazi kubwa iliyofanywa na Dkt. Samia katika kuboresha huduma za kijamii na miundombinu, hivyo wapo tayari kuhakikisha anapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.




Social Plugin