Na mwandishi wetu, Morogoro
Mwanamuziki na mfalme wa mashairi Tanzania, Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele, amewataka Watanzania, hususan vijana, kuacha kuwa na mihemko ya kususia kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza akiwa mkoani Morogoro, Afande Sele amesema vijana wanapaswa kutumia nguvu yao kwa kushiriki kikamilifu katika kupiga kura badala ya kujiingiza kwenye maandamano au matendo yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Amesisitiza kuwa kutokushiriki uchaguzi ni sawa na kujinyima haki ya kikatiba, huku akiwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kutumia kura zao kuamua mustakabali wa taifa.
Afande Sele amesisitiza umuhimu wa vijana kutambua nafasi yao katika kulinda amani, umoja na maendeleo ya taifa, akieleza kuwa ushiriki wao kwenye uchaguzi ni njia halali na ya heshima ya kuleta mabadiliko wanayoyataka.
“Kura yako ni silaha ya mabadiliko. Usiikatae, usiikodishe, na usiipoteze kwa maneno ya mihemko,” amesema Afande Sele.

Social Plugin