
Msanii maarufu wa muziki wa Kiswahili na Makabila kutoka Kenya, Super Star Atommy Sifa Igwee, ametoa wimbo wake mpya wa heshima akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, ukiwa rasmi kwenye video ya 4K iliyotengenezwa na Migera Studio.
Wimbo huo unaonesha shauku na mapenzi ya msanii huyu kutoka Kenya kwa uongozi wa Rais Samia, akibainisha mafanikio na mchango wake katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania.
Video ya “Mama Samia” imetengenezwa kwa ubora wa picha wa 4K, ikionyesha ufanisi wa kisanaa na kipaji cha msanii.
Video hiyo imesambaa kupitia YouTube na tayari imevutia mashabiki wa muziki wa Kiswahili pamoja na wafuasi wa Rais Samia, wakipongeza msanii kwa jitihada zake za kuenzi uongozi wa taifa kupitia sanaa.
Kiungo cha video: Super Star Atommy Sifa Igwee – Mama Samia (Official Video 4K)

Social Plugin