Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, Bw. Joseph Sahani Swalala akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Agosti 4,2025 katika Ukumbi wa Mwadui
Na Sumai Salum - Kishapu
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Bw. Joseph Sahani Swalala, amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuhakikisha wanasimamia mchakato wa uchaguzi kwa weledi, uadilifu na umakini mkubwa, ili kuepuka vurugu na malalamiko katika kipindi chote cha uchaguzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao leo Agosti 4, 2025, katika Ukumbi wa Mwadui Wilayani humo Bw. Swalala amesema wajibu waliopewa ni mkubwa, hivyo unahitaji nidhamu ya hali ya juu na uwajibikaji wa kweli.
"Mmeaminiwa kusimamia zoezi nyeti kwa Taifa, hivyo zingatieni maadili ya kazi hii, fuateni taratibu, msijihusishe na upendeleo wa aina yoyote, na hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa haki hadi mwisho wa uchaguzi," amesisitiza Swalala.
Amewataka kutumia mafunzo hayo kama fursa ya kujiongezea maarifa na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa chaguzi, ili kuhakikisha kuwa kila hatua ya mchakato inatekelezwa kwa ufanisi bila kuibua migogoro au uvunjifu wa amani.
Katika hatua nyingine, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Johanita Projest, amewaapisha wasimamizi hao kwa kiapo maalum cha kutoshiriki au kujiusisha na shughuli yoyote ya kisiasa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mhe. Johanita amewakumbusha kuwa nafasi waliyopewa ni ya kisheria na hivyo wanapaswa kuwa waadilifu, waaminifu, na kutunza siri za kazi wanazozifanya kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
“Kiapo mlichokula ni agano mbele ya sheria na mbele ya jamii. Msikubali kutumika kwa namna yoyote ambayo inaweza kuvuruga uchaguzi au kuvunja amani katika Kata zenu,” ameeleza.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Octoba Mwaka huu, ambapo wasimamizi wasaidizi wa kata ndio kiungo muhimu katika kuhakikisha kila hatua ya mchakato wa uchaguzi inatekelezwa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, Bw. Joseph Sahani Swalala akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Agosti 4,2025 katika ukumbi wa Mwadui

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Johanita Projest akitoa kiapo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Agosti 4,2025 katika ukumbi wa Mwadui wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kujengewa uwezo

Afisa uchaguzi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sigisbert M. Rwezaula akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Agosti 4,2025 katika ukumbi wa Mwadui.

Social Plugin