Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VYAMA 17 VYAIDHINISHWA KUGOMBEA URAIS, ACT WAZALENDO NJE



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Hatimaye, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekamilisha mchakato wa urejeshaji fomu za wagombea wanaowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuidhinisha jumla ya vyama 17 pekee kushiriki katika kinyang'anyiro hicho.

Katika hatua hiyo, Chama cha ACT Wazalendo hakijajumuishwa kwenye orodha hiyo, hivyo kumwondoa rasmi mgombea wake, Luhaga Mpina, katika mbio za urais.

Majina ya wagombea waliopitishwa yamebandikwa leo Agosti 27, 2025, kwenye ubao wa matangazo wa ofisi za INEC jijini Dodoma. 

Kwa mujibu wa tangazo hilo, ACT Wazalendo ni miongoni mwa vyama vilivyoshindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa INEC, Kailima Ramadhan, amebainisha kuwa vyama vilivyopitishwa vimefuata kikamilifu masharti ya kisheria na taratibu za uchaguzi. 

Aidha, amethibitisha kuwa kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi kesho, Agosti 28, 2025.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com