Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SAKALA, SALUM KITUMBO,RAHMA WAENDELEA NA MOTO WA KUSAKA KURA ZA 'NDIYO' WANACHAMA CCM KATA YA MJINI - SHINYANGA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdul Aziz Said Sakala, ameendelea kuonesha ari na dhamira ya dhati kwa kuomba kura za “NDIYO” kutoka kwa wanachama wa CCM ili apeperushe bendera ya chama kwenye nafasi ya Udiwani wa Kata ya Mjini, Jimbo la Shinyanga Mjini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kampeni za Sakala zinaendelea kwa kasi, zikiwa zimechochewa na maamuzi ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kupitia na kujadili majina ya wanachama waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali kupitia mchakato wa kura za maoni ndani ya chama.

Sakala anachuana vikali na makada wengine wa CCM wakiwemo Rahma Kwareri, Nassor Warioba, Abubakar Mukadam, na Salum Kitumbo, ambapo mshindi wa kura za maoni ataibuka kinara na kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao.

Wanachama wa CCM Kata ya Mjini sasa wanasubiri kwa hamasa kubwa kuona nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro hiki kinachoonekana kuwa na ushindani mkali na historia mpya ya kisiasa.












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com