Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Jimbo Kuu Katoliki la Songea limeadhimisha kwa shangwe siku ya Upashanaji Habari sambamba na Jubilei ya miaka 2025 tangu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, katika tukio lililowakutanisha Umoja wa Vijana wa Kanisa hilo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Padri Abate Octavian Masingo – OSB kutoka Abasia ya Hanga, ameeleza kuwa Jubilei ni wakati wa kutoa shukrani kwa Mungu, kuimarisha imani na kujikita katika safari ya kiroho inayoelekea kwenye ukamilifu.
Amesisitiza kuwa licha ya changamoto mbalimbali za kijamii na kimaadili, waumini wanapaswa kuwa thabiti na wenye msimamo katika imani yao na kujiepusha na tamaa ya mafanikio ya haraka yanayowapelekea kuporomoka kimaadili.
Cecilia Moses Migoye, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Jimbo Kuu la Songea, ameeleza kuwa vijana wameadhimisha Jubilei hiyo kwa kuanza na semina zilizowasaidia kupata maarifa kuhusu nafasi yao katika Kanisa na jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha ya ujana.
Cecilia Moses Migoye, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Jimbo Kuu la Songea, ameeleza kuwa vijana wameadhimisha Jubilei hiyo kwa kuanza na semina zilizowasaidia kupata maarifa kuhusu nafasi yao katika Kanisa na jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha ya ujana.Ametoa wito kwa vijana wote kuwa karibu na Kanisa kwani ndilo linatoa ulinzi wa kweli katika maisha yao.
Ameongeza kuwa, mambo mengi ya dunia ni batili endapo hayawapeleki karibu na Kristo.
Kwa upande wake kijana Eric Msemwa kutoka Parokia Takatifu ya Bombambili, amesema kuwa wamepewa mafundisho ya kiroho yamewasaidia kutambua umuhimu wa kumtumikia Mungu katika ujana wao.
Ametoa wito kwa vijana walioko pembezoni kurudi katika imani akisisitiza kuwa kumtumikia Mungu kuna raha ya kipekee.
Amewanukuu wahubiri kwa kusema, "Umkumbuke Muumba wako siku za ujana wako" (Mhubiri 12:1), na kuonya kuwa kutoishi kwa kufuata Neno la Mungu kunaweza kuwaingiza vijana kwenye matatizo kama vile ulevi, matumizi ya dawa za kulevya, na uhalifu.
Amewanukuu wahubiri kwa kusema, "Umkumbuke Muumba wako siku za ujana wako" (Mhubiri 12:1), na kuonya kuwa kutoishi kwa kufuata Neno la Mungu kunaweza kuwaingiza vijana kwenye matatizo kama vile ulevi, matumizi ya dawa za kulevya, na uhalifu.Maadhimisho haya yameashiria mwamko mpya kwa vijana wa Kikatoliki katika Jimbo Kuu la Songea, huku yakielekeza macho yao katika imani, maadili, na huduma ya Kanisa.
Viongozi wa Kanisa wameendelea kutoa wito kwa jamii nzima kushirikiana katika kuwaongoza vijana kuelekea maisha bora ya kiroho na kijamii.


Social Plugin