Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC MASINDI AONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI KISHAPU


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika kuweka mazingira rafiki kwa mama na mtoto ili kuimarisha afya kupitia unyonyeshaji wa maziwa ya mama, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuthamini uhai na maisha ya kizazi kijacho.


Akizungumza Agosti 7, 2025 katika uwanja wa Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya Mhe. Masindi amesema kuwa maziwa ya mama ni hazina ya lishe bora na kinga muhimu kwa watoto wachanga na wachanga zaidi.

“Unyonyeshaji ni suluhisho la msingi kwa afya bora ya mtoto. Maziwa ya mama hayana gharama, huzalishwa moja kwa moja na husaidia kulinda maisha ya mtoto kwa kumpa virutubishi vyote anavyohitaji,” amesema.

Mhe. Masindi amebainisha kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha ya mtoto bila hata maji, na kuendelea hadi mtoto anapofikisha miaka miwili, ni njia bora ya kupunguza udumavu na utapiamlo nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa kitaifa wa mwaka 2022, kiwango cha udumavu mkoani Shinyanga kilipungua kutoka asilimia 32.1 mwaka 2018 hadi asilimia 27.5 mwaka 2022, hatua aliyosema imetokana na jitihada za kuongeza elimu kuhusu lishe bora na unyonyeshaji. 

Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Thamini Unyonyeshaji Weka Mazingira Wezeshi kwa Mama na Mtoto.” DC Masindi amesisitiza kuwa mazingira hayo yanajumuisha kumpunguzia mama mzigo wa kazi, kuhakikisha anapata lishe bora, muda wa kupumzika, chumba maalum cha kunyonyesha kazini na msaada wa kihisia na kiuchumi.

“Mama anapaswa kula milo mitano yenye mchanganyiko wa makundi yote ya chakula, apate muda wa kutosha wa kupumzika, na apewe msaada wa karibu kutoka kwa familia na jamii,” ameeleza.

Amewaasa waajiri kuweka vyumba maalum vya kunyonyesha kazini ili kuwasaidia mama kuendeleza mazoea bora ya unyonyeshaji hata baada ya kurudi kazini.

Mhe. Masindi amesisitiza kuwa kutonyonyesha kuna madhara makubwa kwa mtoto, ikiwa ni pamoja na hatari ya kudumaa kimwili na kiakili, utapiamlo, na kukosa kinga ya mwili. “Mtoto chini ya mwaka mmoja hapaswi kupewa maziwa ya ng’ombe.

Maziwa ya mama yanafaa zaidi kwa ukuaji wa ubongo na kinga ya mwili,” amesema huku akiwasihi wazazi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe.Masindi amewataka viongozi wa jamii, familia na taasisi zote kuendelea kutoa elimu kuhusu faida za unyonyeshaji kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii na kiafya. “Kuthamini unyonyeshaji ni kuthamini maisha.

Tuwe sehemu ya mabadiliko kwa kuweka mazingira bora kwa mama na mtoto,” amesema huku akihimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu
.

Meneja Mradi wa Grow-Enrich unaotekelezwa na shirika la World Vision Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shukrani Dickson akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi

Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Yusuph Hamis, amesisitiza umuhimu wa mtoto kunyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili kusaidia maziwa ya awali (colostrum) kutoka kwa haraka, kwani ndiyo kinga ya kwanza dhidi ya maradhi.

Bw. Yusuph ameeleza kuwa mtoto anapaswa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa chakula wala kinywaji kingine kwa miezi sita ya mwanzo, ili kumkinga dhidi ya maradhi na utapiamlo.

Mkazi wa Kijiji cha Shagihilu, Francis Limbe, amesema kuwa sasa jamii imeanza kupata uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa unyonyeshaji akisisitiza kuwa maziwa ya mama huimarisha afya ya mtoto na hata kumjengea msingi thabiti ya mama yana nguvu kubwa kwa mtoto wa kiume pia yanamjenga kuwa mwanaume kamili mwenye afya na uwezo wa kupata watoto baadaye maishani.

Kwa upande wake, Kwandu Bodigo, mkazi mwingine wa kijiji hicho, ameeleza kuwa kupitia mafunzo yaliyotolewa, wamepata elimu ya kina juu ya lishe bora na faida za kunyonyesha. “Tunaenda kuwa mabalozi wazuri wa elimu hii kwa kina mama wenzetu.

Lengo letu ni kuwa na taifa lenye watu wenye afya njema ya mwili na akili,” amesema kwa msisitizo. Wananchi wengi waliohudhuria maadhimisho hayo walionesha kufurahia elimu waliyopata, huku wakiahidi kuisambaza kwa jamii yao ili kuhakikisha watoto wa Tanzania wanapata mwanzo bora wa maisha kupitia maziwa ya mama.

Kaimu mtendaji Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Godfrey Tesha akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi

Mwenyekiti wa Kijiji cha Shagihilu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Nickson Limbe akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi

Afisa lishe Mkoani Shinyanga Yusuph Hamis akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi
































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com