
Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga ameibuka mshindi wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Kishapu kwa kupata kura 7,814 kati ya kura halali 12,864, na hivyo kuacha wapinzani wake kwa tofauti kubwa.
Bonda Nkinga ameshika nafasi ya pili kwa kura 1,730, akifuatiwa na mbunge aliyemaliza muda wake, Bonophase Butondo, aliyepata kura 1,290. Wagombea wengine ni Doto Kwigema aliyepata kura 597, George Jimisha kura 590, Madaha Chaba kura 503 na John Ngano kura 432.
Jumla ya kura 18,443 zilipigwa katika mchakato huo, ambapo kura 201 ziliharibika.
Social Plugin