Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU 150 WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA BOMBO

 Na Hadija Bagasha Tanga

Waumini wa dini ya Kiislamu zaidi ya 150 Mkoani Tanga wamejitokeza kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga Bombo kwajili ya kuchangia damu ikiwa ni jitihada za kukabiliana na vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu kwa wagonjwa,  wakina mama wajawazito na majeruhi wa ajali. 

Akizungumza na kituo hiki mara baada ya zoezi la uchangiaji damu Mkuu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga Tanzania Sheikh Sajad Hassan,  amesema tukio hilo ni tukio la kihistoria wakiunga mkono yale yaliyofanywa na mjukuu wa Mtume Muhhamad (S.A.W) Immam Hussein,  miaka 1400 iliyopita. 

"Imman Hussein alitoka ili kukataza mabaya,  kukemea mabaya na kuamrisha mema alitoka kumpinga mtawala dhalimu  aliyekuwepo zama hizo Yazid Bin Muayah ndio maana sisi tumekuja hapa kwenye hospitali hii ya Bombo kuja kijitolea damu zaidi ya watu 150 ili kuweza kuwasaidia wagonjwa na wale wasiojiweza tukio hili ni sadaka kutoka kwetu kama vile alivyofanya Imman Hussein kwa kujitolea damu yake nafsi yake,  mali yake yeye na familia yake na sisi tukaona tusikae kimya, "alisema

"Tunawahamasisha waislamu wote kuweza kufanya matukio haya adhimu katika Hospitali kama hizi na hospitali nyingine zote za hapa Nchini kwetu na maeneo mengine ambazo zina watu wanamahitaji ya damu,  zenye wagonjwa wengi kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa, "alisisitiza

Aidha alisema kwamba Taasisi hiyo ya Bilal Muslim Mission imefanya matukio hayo ya kujitolea damu katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo katika Wilaya ya Pangani,  Korogwe ambapo watu wengi wamekusanyika na kuweza kujitolea damu bure bila malipo yeyote bali wamefanya kama sadaka ya kujilea kwajili ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuitika wito wa Immam Hussein mjukuu wa Mtume (S.A.W) aliyeuwawa mwaka wa 61Hijria katika ardhi ya Karbalaa katika Nchi ya Iraq. 

Kwa upande wake Salvatory Lymo Mteknolojia wa maabara hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga Bombo ameishukuu Taasisi ya Bilal Muslim Mission kwa kchangia damu na kutoa misaada mbalimbali kwajili ya wagonjwa waliolazwa ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha hakuna vifo vinavyotokana kwa kukosekana damu. 

"Bilal Muslim imetoa kipaumbele kuhakikisha kwamba hakuna vifo vinavyotokana na kukosekana kwa damu wamekuwa wakitoa ushrikiao wakati wote pale tunapowahitaji wamekuwa wakitusaidia katika suala zima la kuhakikisha benki ya damu salama inakuwa na damu ya kutosha na kuzuia vifo vyote ambavyo vinaweza kutokea kwa kukosekana damu, "alisema Salvatory huyo. 

"Kama tunavyojua damu ni kiungo muhimu sana hivyo tunaendelea kuishukuru Taasisi ya Bilal Muslim na tunahamasisha na taasisi zingne ziige mfano huu ili tuendelee kuwa na damu katika kipindi chote cha mwaka hospitalini kwasababu damu inahitajika kwenye mahitaji ya dharura pekee na nje ya hapo kunakuwa hakuna mbadala ndio maana tunahamasisha jamii,  taasisi nyingine pamoja na watu kujitolea kwenye jambo hili ili kila mwanajamii ahamasike kwa namna ya kipekee kuhakikisha kunakuwa na damu salama ya uhakika, "alibainisha Salvatory. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com