
Na Hadija Bagasha Tanga,
Waislamu Nchini wametakiwa kuitumia siku ya Ashuraa kwa ajili ya kupinga na kukemea matendo maovu ikwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii hivi sasa ambavyo vimekuwa vikigharimu maisha ya watu jinsia zote.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala wa Taasisi ya Bilal Muslim Mkoa wa Tanga Sheikh Abdulrazak Bilal wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume (S.A.W) ambaye ni Imamu Hussein (as).
Amesema kuwa Imamu Hussein ni kielelezo cha kiongozi ambaye alikufa kwa ajili ya kutetea usawa miongoni mwa jamii kwa kupinga vitendo viovu hivyo ni muhimu Waislamu nchini nao wakawa mfano bora wa kutetea vitendo vya kidhalimu.
"Ni wajibu wetu waislamu kuitumia siku ya Ashura kama kielezo cha kupinga vitendo viovu lakini na kuhamasisha matendo mema miongoni mwa jamii ili dunia iweze kubaki mahali salama"amesema Sheikh Bilal.
Kwa upande wake Shafii Mohamed Nina Mkuu wa Taasisi ya Abdul Abas Tanga amesema siku hiyo ya Ashuraa ambayo ni kumbukumbu ya siku aliyofariki dunia alipouwawa kikatili mjukuu wa Mtume.
"Tukio hili tunaomba watu wote walisome na walifahamu vizuri wale ambao wanataka uadilifu wanataka uongozi katika jamii ni lazima upingane na dhuluma laima ujue kila aina ambayo inakwenda kinyume na maadili ya uongozi na ndio maana Imam Ali Hussein alisimama kupinga dhuluma ili aweke mambo sawa, dini iwe sawa, ili dini iwe na amani na ionekane ni ile aloyoileta Mtume Muhamad (S.A.W),"alisisitiza Sheikh Kadhimu Abbas ambaye ni Mkuu wa chuo cha Kiislamu Bilal Muslim Tanga.









Social Plugin