Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU KATIKA VIWANJA VYA SABASABA



MATUKIO KATIKA PICHA




















NA.MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM.

Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake ili kupata elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama SABASABA yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Aidha, wameonesha kuridhishwa na huduma zinazitolewa na ofisi hiyo pamoja na mambo mengine wamepata elimu kuhusu masuala ya vijana, ajira ulemavu na Uratibu wa Shughuli za Serikali.

Maonesho hayo kwa mwaka huu yana Kauli Mbiu inayosema “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa sabasaba, Fahari ya Tanzania” leo tarehe 03 Julai, 2025.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com