Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTAALAM WA AFYA AJITOSA UBUNGE DODOMA MJINI



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Fatuma Waziri amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiahidi kuendeleza mazuri yaliyofanywa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo,Anthony Mavunde.

Fatuma mwenye Elimu ya Shahada ya Uzamili kwenye Masuala ya afya amechukua fomu hiyo leo katika ofisi za CCM,Wilaya ya Dodoma Mjini na kukabidhiwa na Katibu wa CCM,Wilaya hiyo,Sophia Kabibi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu Fatma amesema dhamira yake ni kuhakikisha anaendeleza pale alipoishia aliyekuwa Mbunge wa Dodoma Mjini,Anthony Mavunde kwani amefanya kazi nzuri na ya kutukuka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com